| TANGAZO KWA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2026
Ili kuthibitisha kuwa mwanao atafika yakupasa MZAZI/MLEZI ulipe malipo ya awali ya Tshs. 600,000/= kwa ajili ya nafasi hiyo. Lipa malipo hayo kabla ya tarehe 24 SEPTEMBA, 2025. Fedha hii itakuwa ni sehemu ya ada. Malipo hayo yafanyike kwenye BENKI YA CRDB, TAWI LOLOTE; JINA LA AKAUNTI: THE ORDER OF ST. AUGUSTINE – TAGASTE, AKAUNTI Na. 0150396191300. Risiti ya Benki iletwe shuleni mara baada ya malipo ya benki. Isipoletwa shuleni na kukatiwa risiti ya shule, itaeleweka kuwa malipo hayakufanyika na nafasi yako itachukuliwa na mtu mwingine. MUHIMU: Endapo mwanao hatafika shuleni, fedha hiyo haitarudishwa. Pia ukilipa baada ya tarehe 24 September Mtoto hatopokelewa na pesa haitarudishwa. Usipoilipia nafasi hii itachukuliwa na mtu mwingine na kuanzia tarehe 25 SEPTEMBER, 2025 hutakuwa na haki na nafasi hiyo. UNAPOLETA RISITI KUMBUKA KUFIKA NA MTOTO KWA AJILI YA VIPIMO VYA SALE YA SHULE NA KUCHUKUA JOINING INTRUCTIONS. Tunawatakia maandalizi mema na Karibuni sana St. Augustine Tagaste Secondary School FIKA OFISINI UCHUKUE MAELEZO YA KUJIUNGA (JOINING INSTRUCTIONS) |