MMILIKI WA SHULE

Shule hii ni ya Kanisa Katoliki inayomilikiwa na Shirika la Mtakatifu Agustino (OSA). Shule hii inaenshwa kwa kufuata taratibu zote za Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, yaani sheria ya Elimu Na. 25 ya 1978 na marekebisho yake ya Na.10 ya mwaka 1995.
Shirika la Mtakatifu Agustino liliingia nchini Tanzania mwaka 1976 huko jimboni Songea likitokea huko Ulaya nchini Hispania. Hadi sasa Shirika hili lina Watawa wazalendo (Mapadre na Mabruda) wapatao 28 wanaoishi katika nyumba nne KolaB, Morogoro; Mavurunza; Kimara Suca, Dar es Salaam; na Mkolani – Nyegezi, Mwanza
8
This entry was posted in News. Bookmark the permalink.

Comments are closed.